Monday, October 8, 2012

Biriani Ya Kuku


VIPIMO VYA NYAMA
 
Kuku  1/2 - 1kg  
Chumvi kiasi
Mafuta 1 Kikombe
Samli ½ Kikombe
Kitungu (Kata virefu virefu) 3 Vikubwa
Nyanya (kata vipande) 2
Nyanya kopo 1 Kijiko cha chakula
Thomu 1 Kijiko cha chakula
Tangawazi 1 Kijiko cha chakula
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Pilipili ya unga nyekundu ½ Kijiko cha chai
Kotmiri iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula
Viazi 6
Gram masala 1 Kijiko cha chai
Mtindi ¼ Kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA

  1.     .  Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli.  Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
  2.       Kaanga viazi na viweke pembeni.
  3.       Chukua sufuria tia kuku, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
  4.     Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.



VIPIMO VYA WALI
Mchele 2-3 cups
Hiliki nzima   3
Mdalasini mzima 1
Zafarani ½ kijiko cha chai
Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe
Chumvi kiasi
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.

NAMNA YA KUTAYARISHA
  1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
  2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
  3. Tia hiliki na mdalasini.
  4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
  5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
  6. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
  7. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya kuku.

No comments:

Post a Comment