VIPIMO VYA NYAMA
Kuku 1/2 - 1kg
Chumvi kiasi
Mafuta 1 Kikombe
Samli ½ Kikombe
Kitungu (Kata virefu virefu) 3 Vikubwa
Nyanya (kata vipande) 2
Nyanya kopo 1 Kijiko cha chakula
Thomu 1 Kijiko cha chakula
Tangawazi 1 Kijiko cha chakula
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Pilipili ya unga nyekundu ½ Kijiko cha chai
Kotmiri iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula
Viazi 6
Gram masala 1 Kijiko cha chai
Mtindi ¼ Kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA
- . Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
- Kaanga viazi na viweke pembeni.
- Chukua sufuria tia kuku, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
- Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.
VIPIMO VYA WALI
Mchele 2-3 cups
Hiliki nzima 3
Mdalasini mzima 1
Zafarani ½ kijiko cha chai
Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe
Chumvi kiasi
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.
NAMNA YA KUTAYARISHA
- Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
- Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
- Tia hiliki na mdalasini.
- Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
- Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
- Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
- Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya kuku.
No comments:
Post a Comment